Burudani

#SportsUpdates #KuelekeaLigiKuu2018 Coastal Union kuipiku Mbao FC wakiwa na AliKiba?

#SportsUpdates #KuelekeaLigiKuu2018 Coastal Union kuipiku Mbao FC wakiwa na AliKiba?

Mwaija Salum

August 7th, 2018

No comments

Misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu Bara, timu ya mbao FC ya Mwanza ilifanikiwa kupanda Ligi Kuu Bara na kuleta chachu katika ligi hiyo hasa pale ilipokuwa ikikutana na timu kubwa za Yanga, Simba na Azam na kusababisha timu hizo kutumia nguvu za ziada ili kupata matokeo kwa Mbao FC.
.
Katika msimu huu wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza tarehe 22 Agosti, timu ya Coastal Union ‘Wagosi Wa Kaya’ ya jijini Tanga wamerejea tena kwenye ligi hiyo baada kusota misimu miwili katika ligi daraja la kwanza wakiingia kwa staili mpya ambayo haijawahi kutokea kwa kumsajili msanii maarufu wa Bongo Fleva, @OfficialAliKiba kuongoza mashambulizi katika timu hiyo.
.
Msanii huyo tayari ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa timu hiyo na hivi karibuni Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union, Steven Mnguto alisema msanii huyo amependa kuichezea timu yao kwa mapenzi yake na wamemkaribisha kwa mikono miwili.

Je Unadhani Coastal Union itaipiku Mbao chini ya mchezaji machachari, Ali Kiba?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966