Burudani

Mzee Majuto kuzikwa kesho kwao Tanga

Mzee Majuto kuzikwa kesho kwao Tanga

Mwaija Salum

August 9th, 2018

No comments

Mwigizaji Mkongwe, Marehemu King Majuto anatarajiwa kuzikwa kesho kwao jijini Tanga, mwigizaji huyo alifariki jana majira ya saa moja jioni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za awali kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Algaesha, jana  zilisema hali ya King Majuto ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la  Sewahaji kwenda  ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni ya jana hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa mbili alikata roho.

UTARATIBU WA KUMUAGA MZEE WETU KING MAJUTO.

Mwili wa Marehemu Mzee wetu Majuto utaswaliwa na kuagwa katika Msikiti ulipo pale ndani Muhimbili wakti wa Swalat Dhuhr ( Swala ya Mchana).

BAADA YA HAPO MWILI UTAAGWA VIWANJA VYA KARIMJEE.

HIVYO, Kuanzia saa nane Mchana Wanafamilia wote, ndugu, jamaa na marafiki, Wapenzi na Wadau mbali mbali tunatakiwa tukutane pale kwa ajili ya Kusoma Dua na Kumuaga Mzee wetu.

Baada ya Swalat L’laasir (Swala ya Alasiri ) Mwili wa Marehemu Mzee wetu Majuto utasafirishwa kwenda Mkoani Tanga na Maziko ni Ijumaa baada ya Swalat Dhuhr ( Swala ya Mchana ) Tanga Mjini.

Pia kutakuwa na Usafiri maalum kwa ajili ya Wasanii.

Wote mnaotarajia kusafiri Mnaelekezwa kujiorodhesha kwa Afisa Habari wa TDFAA Kinondoni Bw. Masoud Kaftany.

Michango yote itakusanywa na Kamati ya Matukio na Uratibu.

By. Chiki Mchoma.
Mwenyekiti/Uratibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966