Kitaifa

Uhamiaji: Msisubiri Mhamiaji Haramu agombee ubunge ndio utoe taarifa!

Uhamiaji: Msisubiri Mhamiaji Haramu agombee ubunge ndio utoe taarifa!

Mwaija Salum

August 9th, 2018

No comments

Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wananchi kutoa taarifa Uhamiaji kuwa kuna mtu fulani sio raia wa Tanzania baada ya mtu huyo kuwa na nia ya kugombea nafasi fulani ya uongozi kama ubunge, udiwani au urais.

Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda kupitia kipindi cha #Clouds360 cha #CloudsTV amewataka Watanzania wasisubiri mhamiaji haramu agombee nafasi yoyote ya uongozi ndio watoe taarifa kwenye Idara hiyo.

‘’Wananchi ndio wenye wajibu wa kuilinda nchi yao dhidi ya uvamizi wowote ule, suala la kutambua nani ni raia wa Tanzania na sio raia ni la wananchi, mara nyingi huwa tunapokea taarifa kipindi ambacho huwa kuna matukio, kuna mtu anataka kugombea ubunge ndio taarifa zina kuja kwetu kuwa sio raia wakati alikuwa anaishi muda mrefu, au anapatiwa kipande cha ardhi analima baada ya mazao yake kustawi ndio taarifa zinakuja kwetu kuwa sio raia’’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966