Burudani

Nilishafanya maamuzi magumu kuhusu mavazi yangu-Chemical

Nilishafanya maamuzi magumu kuhusu mavazi yangu-Chemical

Mwaija Salum

September 14th, 2018

No comments

Rapper Chemical amesema kuna kipindi alikuwa akipata wakati mgumu sana kuhusu mavazi yake, kuna watu walikuwa wakimshauri avae nguo za kike na wengine wakimwambia avae za kiume, ila yeye alifanya maamuzi magumu ya kuwasikiliza mashabiki wake.

‘’Nimeshavaa tofauti sana mbona kwenye video zangu nyingine nilivaa ktofauti kama vile watu walivyokuwa wanataka, ila watu wameshanizoea kila wakiniona navaa nguo za kiume lakini naweza kuvaa nguzo zozote zile lakini pia mpaka nimekuwa na mwonekano huu kwasababu nimeshajaribu mwonekano mwingine nikaona jinsi gani watu walivyonipokea, hawakuupenda walitamani nibaki kwenye mwonekano wangu waliouzoea’’ Alisema Chemical alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao wa Cloudsfm.co.tz

’Unaangalia mashabiki wanataka nini ni kitu ambacho walikupokea nacho, nilivyovaa kikike na kupaka ‘makeup’ nilipata maoni mengi kutoka kwa mashabiki wangu wa mitaani wakimtaka Chemical huyu ambaye unamwona sasa hivi anayevaa kiume’’ Alisema Chemical.

‘’Mwanzoni ilikuwa ikiniumiza akili sana, watu wangu wa karibu walikuwa wakiniambia nivae ‘kiugumu’ au nguo za kike kwakuwa mimi ni mwanamke ilikuwa ikinisumbua sana, niliamua kuwasikiliza mashabiki wangu’’ Aliongeza Chemical.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966