Burudani

Mmbeya asiyejulikana awachonganisha Dj D Ommy, Dj Zero, Dj Sinyorita na Dj Mafuvu

Mmbeya asiyejulikana awachonganisha Dj D Ommy, Dj Zero, Dj Sinyorita na Dj Mafuvu

Mwaija Salum

October 9th, 2018

No comments

Dj Mafuvu ambaye wiki kadhaa zilizopita alikuwa mmoja wa Madj waliopata mwaliko na Clouds FM wa kupiga kwenye kipindi cha XXL alizua gumzo kwenye mtandao baada kuwatuhumu baadhi ya madj wa Clouds FM ambao ni Dj Dommy, Dj Sinyorita, Dj Zero, Dj Feruuh na Dj Bulla kuwa anam’sinch’ ili asipate ‘mchongo’ kwenye redio hiyo.
.
‘’Nilipenyezewa’ info’ na mtu ninayemwamini sana , daah nilishangaa kwa sababu Dj Dommy ni kijana wangu nilimtengeneza mwenyewe, na Dj Zero nafahamiana naye kwa muda mrefu na madj wengine nafahamina nao pia, sasa nilivyosikia kuwa wanafanya kampeni nisifike mjengoni sikujisikia poa, nikamwaga povu kama loteee’’ Alisema Dj Mafuvu alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kwenye shindano maalum kwa ajili ya kuwashindanisha madj ambapo mshindi atakayechaguliwa na wasikilizaji atakinukisha kwenye Tigo Fiesta kwenye mikoa ya Songea na Mtwara.
.
‘’Nipo mjengoni leo,nawashukuru sana Clouds na mashabiki ambao wamekuwa wakinipush sana kurudi kwenye media’’ Alisema Dj Mafuvu. Angalia video Dj Mafuvu alivyokutana na Dj Dommy studio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966