Burudani

Dk Cheni akosa hamu ya kutazama Bongo Movie.

Dk Cheni akosa hamu ya kutazama Bongo Movie.

Mwaija Salum

November 6th, 2018

No comments

Takribani miaka mitano sasa tangu msanii wa siku nyingi wa filamu za Kibongo, Dk Cheni aache kufanya filamu, msanii huyo afunguka kukosa hamu ya kutazama filamu za sasa hapa nchini.

‘’Sijafanya filamu kwa muda mrefu zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa sababu ya kukosekana kwa soko la kuuza filamu hapa nchini’’ Alisema Dk. Cheni alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao wa Cloudsfm.co.tz

‘’Soko la filamu kwa sasa limenifanya niachane na masuala ya kuigiza, hata hizi filamu zinazochezwa sasa hivi sijapata bahati ya kuziangalia, unajua unakosa hamu za kuzitazama kwa sababu soko hujalijua liko wapi, ukilijua soko lilipo tunaangalia hizo filamu ili tupate kitu kizuri zaidi ya yule tuliyemwangalia kama huna cha kuuza huwezi kuwa na hamu ya kuuza’’ Aliongeza Dk. Cheni

‘’Kwa sasa nashi kwa kutegemea kazi yangu ya UMC’’ Alisema Dk. Cheni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966