Burudani

Soko la kuuza Bongo Movie lipo, labda halimridhishi Dk. Cheni- Mtitu.

Soko la kuuza Bongo Movie lipo, labda halimridhishi Dk. Cheni- Mtitu.

Mwaija Salum

November 8th, 2018

No comments

Kauli aliyoitoa Dr. Cheni kuhusu kukosa hamu ya kutazama filamu za sasa za hapa nchini, imemwibua msanii wa filamu hizo, William Mtitu na kusema kuwa kauli aliyoitoa msanii huyo alitakiwa awafikirie mashabiki na wasanii wengine wanaoendelea kufanya filamu hizo.

‘’Yeye amesema haangalii filamu, kuangalia ni kitu kingine na kuacha kufanya filamu ni kitu kingine, huoni kwamba ana matatizo? Kwa hali ya kawaida filamu ndio iliyomfanya akaitwa Dk. Cheni, kama yeye ni msanii mkubwa ilitakiwa azungumze kuhusu changamoto zinaoikabili tasnia ili serikali wazione’’ Alisema Mtitu alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mtandao wa Cloudsfm.co.tz

‘’ Anavyosema haangalii hizo sinema kwahiyo anataka na mashabiki waache kuziangalia, vipi kuhusu wasanii wengine wanaoendelea kufanya filamu kwahiyo na wao waache kwa vile hazinunuliki, alichokizungumza si kauli ya kifikra kwa ajili ya kuisadia tasnia na kuwasaidia wengine, yeye kwa sasa hivi anafanya U-MC ndipo anapopatia hela lakini kuna wengine tunategemea filamu kuendesha maisha yetu lazima awafikirie na wengine tulibaki kwenye tasnia hii’’ Aliongeza William Mtitu

‘’Kwahiyo mimi sasa hivi nikisema Ma- MC wa hapa nchini hakuna anayejua wote wababaishaji atajisikiaje?’’  Soko la kuuza filamu lipo ndio maana kuna wasanii bado wanafanya filamu labda yeye halimridhishi’’  Alisema Mtitu.

‘’Soko la filamu lipo ingawa sio kubwa kama zamani, sinema zetu bado zinanunuliwa Kariakoo, watu wananunua filamu zetu, JB bado anafanya filamu na anauza kama kawaida’’ Aliongeza Mtitu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966