Burudani

Ng’ombe mkubwa zaidi ashindwa kuuzwa mnadani.

Ng’ombe mkubwa zaidi ashindwa kuuzwa mnadani.

Mwaija Salum

November 30th, 2018

No comments

Ng’ombe mkubwa zaidi nchini Australia na pengine duniani kote aitwaye Knickers, ameshindwa kuuzika mnadani kutokana na ukubwa wake ambapo wanunuzi wa ng’ombe wa kuchinjwa walikataa kumnunua.

Walisema ni mkubwa mno kiasi kwamba hawezi kutosha kwenye vichinjioni, atawapa taabu tu, akarejeshwa nyumbani.

Hatachinjwa tena na ataishi maisha yake yaliyosalia katika shamba la kuwafuga ng’ombe wa kuchinjwa la Ziwa Preston eneo la Myalup, 136km (maili 85) kusini mwa mji wa Perth.

Ni kama jitu anaposimama pamoja na ng’ombe wengine malishoni au kwenye zizi, ni ng’ombe mnene ajabu. Knickers kwa Kiingereza maana yake n i suruali ya ndani ya mwanamke.

Uzito wake ni  kilo 1,400kg na kimo chake 194cm (6ft 4in).

Alishahasiwa, maana kwamba hawezi kutungisha mbegu. #Picha #DailyMail.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966