Uncategorized

Mai ampandisha ndege Anko Zumo kwa mara ya kwanza.

Mai ampandisha ndege Anko Zumo kwa mara ya kwanza.

Mwaija Salum

November 30th, 2018

No comments

Mwigizaji wa filamu za Vichekesho, Anko Zumo amefunguka mtoto wake Mai Zumo ndiye aliyemfanya apande ndege kwa mara ya kwanza tangu kuzaliwa hivi karibuni kuelekea Dodoma kutokana na sanaa anayoifanya mtoto huyo kwa uwezo mkubwa na wadau mbalimbali kuwapa dili.

‘’Mungu alichotujaalia kikubwa ni safari yetu ya kwenda Dodoma hivi karibuni kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, nilikuwa sijawahi kupanda ndege tangu kuzaliwa na hii yote kwa sababu ya mtoto wangu mwigizaji Mai kwa sababu tumefanya kitu cha tofauti kuigiza pamoja na Mai wengi wa mashabiki wetu wanamtazama zaidi mtoto wetu” Alisema Anko Zumo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Cloudsfm.co.tz

‘’Nilikuwa nahofia kutokana na stori za watu wengine waliokuwa wakisema ukipanda ndege unaweza kutapika, lakini niliona raha sana’’ Aliongeza Anko Zumo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966