Burudani

Mitaji ya biashara, nyumba zangu zimetokana na Clouds- Nay Wa Mitego.

Mitaji ya biashara, nyumba zangu zimetokana na Clouds- Nay Wa Mitego.

Mwaija Salum

December 3rd, 2018

No comments

Wakati jana Dec.2,  Clouds FM ikitimiza miaka 19 ya kuzaliwa, Rapa Nay Wa Mitego ametoa shukrani kwa Clouds FM kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata ambayo yametokana na mchango mkubwa wa Redio ya Watu.

‘’Clouds imenisaidia kwa kiasi kikubwa sana, wakati naanza nilikuwa sisikiki kwenye muziki sikuwahi kuamini kama ninaweza kufanikiwa kwa kiasi hichi, moja kati ya mafanikio yangu kwamba Nay amepiga hatua hii ni Clouds ambayo ina mchango mkubwa sana kupitia tamasha la Fiesta, nimefanya shoo za Fiesta mfululizo kwa miaka mitatu kwa mikoa yote nilipewa pesa yangu ‘cash’ biashara zangu ninazofanya mitaji yake inatokana na Clouds na nyumba zangu nilizojenga zimetokana na mchango mkubwa wa Clouds kupitia shoo za Fiesta, hii ni moja ya sehemu ambayo naiheshimu sana kwenye kazi yangu’’  Alisema Nay Wa Mitego alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao wa Cloudsfm.co.tz

‘’Clouds bado ni Namba Moja’’  Alisema Nay Wa Mitego.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966