Burudani

CLOUDS ILIANZA KWA MKOPO WA MILIONI 40.

CLOUDS ILIANZA KWA MKOPO WA MILIONI 40.

Mwaija Salum

December 4th, 2018

No comments

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema kuwa Clouds FM ilianza kwa mkopo wa Milioni 40 kutoka kwenye benki ya CRDB.

Ameyazungumza hayo kwenye kipindi maalum cha maadhimisho ya miaka 19 ya kuzaliwa kwa Clouds FM.

“Nimshukuru sana Marehemu mama yangu kwani mtaji wangu wa kwanza ulitokana na ufugaji wa kuku. Mtaji huo ndiyo ulitupatia pesa ya tiketi (Mimi na #RugeMutahaba) kutafuta wawekezaji nje”Alisema Joseph Kusaga.

Anasema kwa kuwa yeye na Ruge walionekana vijana wadogo, ilikuwa ngumu sana kupata muwekezaji.

Ndipo Kusaga anaweka wazi kwamba anamshukuru sana Dr Charles Kimei (aliyekuwa Mkurugenzi wa CRDB) kwa sababu yeye aliwasaidia sana kupata mkopo wa milioni 40.

Kusaga anasema maisha yake yote anamheshimu Mzee Kimei kwa sababu pesa hiyo ya mkopo ndiyo ilikuwa muhimili katika mtaji pamoja na mchango mkubwa wa Baba yake (Marehemu Chief Kusaga) ambaye wakati huo alikuwa amestaafu. Anasema baada ya kuona jitihada binafsi za Joseph Kusaga na Ruge, Mzee Kusaga aliamua kuwasaidia fedha na hapo ndipo Clouds ilisimama.
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966