Burudani

Ruge Mutahaba anaendelea vizuri.

Ruge Mutahaba anaendelea vizuri.

Mwaija Salum

December 4th, 2018

No comments

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema Mjumbe aliyetumwa na Clouds kwenda nchini South Afrika amesema Mkurugenzi wa Vipindi Na Uzalishaji, RugeMutahaba anaendelea vizuri.

Amesema kwamba aliona watu wakiuliza kwa nini Clouds Media Group haijaongea chochote kuhusu kuumwa kwa Ruge lakini amewataka watu kufahamu kwamba hilo lilitokana na matakwa ya familia ya kina Mutahaba.

“Baba na Mama mzazi wa Ruge pamoja na familia ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu afya yake, hivyo tusingeweza kuongea chochote bila ruhusa yao” Alisema Joseph Kusaga alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi maalum ya maadhimisho ya miaka 19 ya kuzaliwa kwa Clouds FM.
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966