Burudani

Tigo Fiesta kufanyika Dar – Kusaga.

Tigo Fiesta kufanyika Dar – Kusaga.

Mwaija Salum

December 5th, 2018

No comments

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema kuwa tamasha la Tigo Fiesta jijini Dar es Salaam litafanyika kabla ya kuisha kwa mwaka huu 2018.

“Tigo Fiesta 2018 ipo, na lazima ifanyike kabla ya mwaka kuisha, nimezungumza hadi na Mh Rais Dkt John Magufuli kwamba pengine suala ni ‘venue’, hili jambo limepenyezwa kwa viongozi wa serikali tumekaa tumezungumza..” Alisema Joseph Kusaga alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV katika mahojiano maalum ya kuadhimisha miaka 19 ya Clouds FM.

”Clouds Media Group inazungumza na serikali na wadau wengine wa burudani ili tupate eneo kuweza kujenga ukumbi maalum wa matamasha makubwa.

Kusaga amesema hilo litaepusha kushindikana/kuahirishwa kwa matamasha makubwa kama ilivyotokea kwa Tigo Fiesta 2018 Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966