Burudani

Shilole ahamia kwenye mjengo wake, aishukuru Clouds

Shilole ahamia kwenye mjengo wake, aishukuru Clouds

Mwaija Salum

December 5th, 2018

No comments

 

Kwa mara ya kwanza msanii wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka kuwa mgahawa wake wa Shishi Food na mjengo wake mpya uliopo eneo la Majohe aliohamia mwezi mmoja uliopita vyote vilitokana na Clouds.

 

‘’Nyumba mpya niliyojenga eneo la Majohe, jijini Dar es Salaam, kiwanja nilinunua hela ya Clouds kupitia tamasha la Fiesta, hata Shishi Food ilifunguliwa kutokana na shoo hizo za Fiesta nilifanya kwa miaka minne mfulululizo’’ Alisema Shilole alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mtandao wa Cloudsfm.co.tz katika maadhimisho ya miaka 19 ya kuzaliwa kwa Clouds FM.

‘’Mchango wa Clouds FM ni mkubwa sana kwangu tangu naanza sanaa yangu walinipa msaada mkubwa, ni redio iliyowasaidia wasanii/ watu wengi sana, wasanii wote unaowaona walianzia hapo, hii ni redio Mama na bado inafanya vizuri’’Aliongeza Shilole

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966