Burudani

Nani wa kupinga? Mafanikio yote haya niliyonayo yametokana na Clouds- Chege.

Nani wa kupinga? Mafanikio yote haya niliyonayo yametokana na Clouds- Chege.

Mwaija Salum

December 6th, 2018

No comments

Msanii wa Bongo Fleva, Chege Chigunda amesema hakuna wa kupinga kuwa mafanikio aliyonayo sasa hivi yametokana na Clouds FM.

Ameyazungumza hayo kwenye mahojiano maalum na mtandao wa Cloudsfm.co.tz katika maadhimisho ya miaka 19 ya kuzaliwa kwa Clouds FM.

‘’Naweza kuongea sasa hivi hadi jioni nisimalize, kwa sababu nimefanya muziki kwa muda mrefu sana na mchango wa Clouds na Fiesta kwangu mimi hakuna anayeweza kuupinga ni kitu ambacho kiko wazi na familia yangu inajua na mama yangu (Mama Said) anaishukuru Clouds kila siku kwa mafanikio haya’’  Alisema Chege Chigunda

‘’Tamasha la Fiesta limenitengenezea nyumba yangu ninayoishi na nyinginezo, nilikuwa nikimaliza kufanya shoo nachukua pesa zangu Mill. 18 au 20 naenda kushoot Afrika Kusini’’

‘’Bado naiona Clouds kwa miaka miaka mingi kwa sababu ina sifa ya kuchukua watu wenye ‘talent’ haijalishi ni kipaji cha kusomea au kutoka mtaani, na bado ni Redio namba moja na sisi wasanii tunaiangalia kwa jicho kubwa sana kwa mafanikio yatu ya kimaisha na kimuziki’’ Alisema Chege Chigunda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966