Uncategorized

Mwanamke ana watoto 21, ujauzito wa kwanza aliupata akiwa na miaka 13.

Mwanamke ana watoto 21, ujauzito wa kwanza aliupata akiwa na miaka 13.

Mwaija Salum

January 8th, 2019

No comments

Mwanamke mmoja mwenye watoto 21 amewashangaza watazamaji wa TV baada ya kuweka wazi ya kwamba ujauzito wake wa kwanza aliupata akiwa na miaka 13 tu. Na mwanaume aliyempa ujauzito wakati huo ambaye sasa ni mume wake alikuwa na miaka 18.

Mwanamama huyo ambaye jina lake halisi ni Sue Radford aliyasema hayo kwenye kipindi cha TV kinachoitwa Kid’s and Counting kinachorushwa kupitia channel 4 televisheni ya Uingereza. Baada ya kuweka wazi ya kwamba mtoto wake wa kwanza alimpata akiwa na umri gani watu wote waliokuwepo pale walishtuka kuanzia familia mpaka marafiki hakuna aliyeweza kuamini kirahisi ya kwamba mama huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 43 alipata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 13.

Moja kati ya marafiki zake wa karibu anaitwa Chloe nae alikuwepo kwenye kipindi na alimtania Bi. Sue ya kwamba ilifika mahali aliona hakuna haja ya kumwambia kuhusiana na swala la uzazi wa mpango. Na mmoja kati ya watoto wa kiume wa Sue Radford anitwa James alisema anashindwa kuelewa ni kitu gani kinaendelea kati ya wazazi wake kwani mpaka sasa watoto wapo 21 na hajui ni lini mama yake ataacha kuzaa.

Pamoja ya kwamba watu wengi walishtushwa na historia ya Sue Radford kupata ujauzito akiwa na miaka 13 na mume wake alikuwa na miaka 18 wakati huo. Bi. Sue mwenyewe anadai ilimchukua dakika 12 tu labour mpaka kupatikana mtoto wake huyo wa kwanza.

Source: Daily Mail

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966