Yanga

Uncategorized

Davido atuhumiwa kwa udhalilishaji wa kingono kwa wanawake!

Davido atuhumiwa kwa udhalilishaji wa kingono kwa wanawake!

Mwaija Salum

January 8th, 2019

No comments

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Davido amejikuta katika wakati mgumu baada ya mwandishi wa habari kutoka nchini humo Kemi Olunloyo kumtuhumu msanii huyo kujihusisha na vitendo vya kuwadhalilisha wanawake kingono yeye pia akiwa ni mhanga wa kitendo hicho alichofanyiwa na msanii huyo.

Hayo yamekuja baada ya msanii Davido kuandika ujumbe katika mtandao wake wa Twitter wakumponda mwanamuziki R Kelly ambaye amekuwa akihusishwa na vitendo vya kuwadhalilisha wasichana wenye umri mdogo ndipo mwanadada huyo alipoibua hoja hiyo.

Kemi alienda mbali zaidi na kusema msanii huyo amekuwa akijihusisha na mambo ya ushirikina na hivyo yeyote aliyemfollow msanii huyo katika mitandao ya kijamii atakuwa ni mshirikina tu.

Kemi na Davido wanadaiwa kutokuwa na maelewano mazuri kwa muda sasa kutokana na ishu za kikazi hivyo huenda Kemi akawa amefanya hivyo kwa ajili ya kutaka kuchafua brand ya Davido.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966