Burudani

Kosa kubwa ni kumtazama cheetah machoni! -Rachel

Kosa kubwa ni kumtazama cheetah machoni! -Rachel

Mwaija Salum

January 9th, 2019

No comments

‘’Nilikwenda Zambia kikazi lakini nii’enjoy’, ilikuwa ni project ya wildlife, ishu ya kumshika Duma (mnyama aina ya Chui) na kupiga naye picha haikuwa rahisi, nilikuwa naogopa wale ni Chui wenye mafunzo lakini sio kwamba wametolewa meno na kucha au sio wakali na hawang’ati , kabla ya kumshika yule Chui tulipewa mafunzo jinsi ya kumshika’’ Alisema mwigizaji Rachel alipokuwa akifanya mahojiano maaluma na mtandao wa Cloudsfm.co.tz

‘’Sio kwamba nilikuwa jasiri kiasi kile na wakati mwingine nikiangalia zile picha siamini, kuna wenzangu walishindwa kumshika kabisa walikuwa wanaogopa, binafsi napenda sana wanyama mara kwa mara huwa nakwenda kutalii mbugani Serengeti , nilichojifunza ni kuwa wanyama na binadamu wanaweza kuishi pamoja bila kuogopeana na kudhuliana na kuheshimiana na kutunziana mazingira’’ Alisema Rachel

‘’Mnyama anaweza kumdhuru mwanadamu kwa kujihami kuwa anaweza kumdhuru kwahiyo anakuwahi, tulipokwenda Serengeti wale ‘Tour Guide’ walituambia mnyama kama Duma ana urafiki sana binadamu lakini lazima uwe mpole kwake, usiwe mwoga na usiangaliane naye machoni ukimwangalia ndio kitu kibaya kuliko kitu chochote atakujeruhi’’ Aliongeza Rachel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966