Michezo

RABBIN SANGA AITWA SERENGETI BOYS

RABBIN SANGA AITWA SERENGETI BOYS

Mwaija Salum

February 8th, 2019

No comments

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Ammy Ninje amesema amevutiwa na kiwango kilichooneshwa na nyota wa Ndondo Cup Academy Rabbin Sanga ambaye anafanya majaribio kwenye klabu ya Besiktas nchini Uturuki.

Ninje amesema, Sanga atakaporudi nchini atajumuishwa kwenye kikosi cha Serengeti Boys kwa ajili ya safari ya Uturuki ambapo timu hiyo itaenda kushiriki mashindano ya vijana wenye umri huo yakiwa ni maalum kwa ajili ya maandalizi ya kombe la vijana Afrika.
“Rabbin nimemuona, nimeona video zake sasa mimi bahati nzuri ni mkurugenzi na vilevile ni mwalimu, kwa hiyo nitamwita baada ya kurudi Jumapili au Jumatatu aje kuungana na timu yetu ya Serengeti Boys.”
“Mtu yeyote ambaye amejitoa mwenyewe kwenda nje ya Tanzania kujaribu, zawadi ambayo sisi tunampa ni kuthamini uwezo wake na uzoefu alioupata kule (nje ya nchi) kwa hiyo akirudi aje ajiunge na Serengeti Boys nadhani itakuwa mwamko kwa vijana wengine wenye umri kama wake kwenda kujaribu nje ya Tanzania.”
“Kiufundishaji ukiangalia psychology part yupo vizuri kwa kitendo cha kutoka Tanzania kwenda nchi ya watu na kufanya vizuri sisi lazima tujaribu kumtengenezea njia ili wakati mwingine ikitokea fursa kama hiyo tayari anakuwa mchezaji wa kimataifa.”
“Amefanya vizuri ukiangalia kwenye nafasi anayocheza anavyopokea mpira na kutoa pasi, yuko busy ana uwezo wa kucheza one vs one kuna vitu vingi ambavyo tayari anavyo sasa sijui mwalimu wake alikuwa nani lakini kwa video fupi nilizoziona ni mtu ambaye anaweza kutusaidia baadaye.”
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966