Burudani

Sijawahi kuhonga, naamini yapo mapenzi bila Pesa –Marioo
Mkali wa ngoma ya Ifunganya, Marioo amedai kuwa hajawahi kuwa na mpenzi ‘mpenda pesa’ na hajawahi kuwa kwenye mahusiano na kutumia kiasi kikubwa cha pesa na baadae akajutia!
Msanii huyo ameyazungumza hayo kwenye mahojiano na mtandao huu wa Cloudsfm.co.tz.
‘’Naamini yapo mapenzi bila pesa, mwanaume hana kitu na mwanamke anampenda na anamvumilia hivyo hivyo japo kwa asilimia chache japo kwa asilimia chache sana naamini kwamba mapenzi ya kweli yapo bila pesa kwa sababu mifano ipo na naiona’’. Alisema Marioo
‘’Sijawahi kuwa na mpenzi anayependa pesa na sijawahi kuhonga, na kitendo hicho ni kumpa pesa msichana kwa sababu unahitaji kutu fulani kutoka kwake, ipo kumsaidia msichana pesa ambayo ni tofauti na kuhonga’’. Aliongeza Marioo
‘’Sijawahi kukaa kwenye mahusiano hadi nikumbuke nilitumia kiasi gani kikubwa cha pesa nikajuta’’ Alisema Marioo