Blog

Mrembo akumbwa na ugonjwa wa ajabu, adondoka na kupasuka.

Mrembo akumbwa na ugonjwa wa ajabu, adondoka na kupasuka.

Mwaija Salum

March 14th, 2019

No comments

Mrembo Emjaye Bowman, mkazi wa Birmingham, Uingereza amekuwa akisumbuliwa na majeraha pamoja na matatizo ya kupooza hii ni baada ya kuanguka na kupasuka sehemu za usoni akiwa kwenye eneo linalotumka kupiga muziki mgahawani.

Ilikuwa ni mwaka 2006 ambapo Emjaye Bowman mwenye umri wa miaka 33 alikimbizwa hospitalini baada ya ajali. Alipopata matibabu aliruhusiwa kurudi nyumbani lakini haikuishia hapo kwani aliporudi nyumbani alianza kusumbuliwa na matatizo ya kichwa , kupoteza fahamu na hata kupungua mwili.

Madaktari wanaosimamia matibabu Ms Bowman wanasema mwanamke huyu amepatwa na matatizo ya kisaikolojia ambayo yanashangaza na hayaelezeki kwani kuna wakati mwili wake huwa unakosa mawasiliano.

Maisha ya Emjaye Bowman yameharibika sana kwani toka wakati huo amekuwa anashindwa hata kutoka nyumbani kwa sababu tu ya aina hiyo ya ulemavu usioonekana.

Lakini kuna mmoja kati ya watu wenye ubunifu kwenye uandishi alisema amegundua ya kwamba watu wenye matatizo ya aina hii huwa wanahitaji tiba ya muziki na mashairi alisema hali hii itamuondolea maumivu na kumfanya yeye kuwa huru.

Daily Mail

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966