Michezo

Kepa aipeleka Chelsea fainali ya Europa League, kucheza na Arsenal.

Kepa aipeleka Chelsea fainali ya Europa League, kucheza na Arsenal.

Mwaija Salum

May 10th, 2019

No comments

Kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga akiokoa penalti ya Goncalo Paciencia kabla ya Edin Hazard kuifungia The Blues penalti ya mwisho Uwanja wa Stamford Bridge mjini London na kutinga fainali ya UEFA Europa League kwa ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 2-2 ndani ya dakika zaidi ya 210 kwenye mechi mbili kali za nyumbani na ugenini. Chelsea ilitangulia kwa bao la Ruben Loftus-Cheek dakika ya 28, kabla ya Luka Jovic kuisawazishia Eintracht-Frankfurt dakika ya 49.

Waliofunga penalti za Chelsea ni Ross Barkley, Jorginho, David Luiz na Hazard wakati Cesar Azpilicueta alikosa na za Eintracht-Frankfurt zimefungwa na Sébastien Haller, Jovic na Jonathan de Guzmán huku Martin Hinteregger na  Gonçalo Paciência wakikosa. Fainali itawakutanisha Arsenal na Chelsea Uwanja wa Bakı Olimpiya mjin Baku, Azerbaijani PICHA ZAIDI SOMA HAPA 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966