Yanga

Michezo

Ndondo Cup 2019 hatua ya makundi kuzinduliwa leo Ijumaa.

Ndondo Cup 2019 hatua ya makundi kuzinduliwa leo Ijumaa.

Mwaija Salum

June 7th, 2019

No comments

Michuano ya Ndondo Cup 2019 hatua ya makundi (32 bora) itazinduliwa leo Ijumaa Juni 7, 2019 kwa bonge moja la game Keko Furniture vs Toroli Kombaini ‘Keko derby’.

Timu hizi ni majirani, zinatenganishwa na barabara tu. Keko Furniture ambayo ni timu ya wauzaji wa furniture mbalimbali za nyumbani na ofisini wanasema, Toroli la kusukumia mbao tu mtu hawezi kununua furniture abebe kwenye toroli. “Sisi ndio matajiri.”

Upande wa pili nako (Toroli Kombaini) wenyewe wanajitapa kwamba wao ndio mafundi bila wao Keko Furniture watakimbia mji waende shamba kulima.

Balaa liko hapa, aliyekuwa Katibu Msaidizi wa Keko Furniture amechomoka ameenda Toroli Kombaini, kwa hiyo anasema mbinu zote za ushindi zinazotumiwa na Keko Furniture anazijua nje na ndani.

Keko derby ni kama derby ya Liverpool na Everton timu zote za mtaa mmoja, mashabiki wote wanatoka mtaa mmoja wanaenda uwanjani kuangalia mbungi.

Sasa unaambiwa hivi, wakazi wa Keko leo ndio siku ya kufua nguo unazianika halafu hakuna haja ya kuzilinda…masela wooote watakuwa uwanja wa Bandari kushuhudia derby ya Keko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This Website is Designed and Developed by Desy Ernest | desy@setuptz.com | 0719955966